<?xml version="1.0" encoding="UTF-8"?><song><lyrics>[V1]
 Bwana Mungu, nashangaa kabisa
 Nikitazama kama vilivyo
 Nyota, ngurumo, vitu vingi vyote
 viumbwavyo kwa uwezo wako.

[V2]
 Roho yangu na ikuimbie
 Jinsi Wewe ulivyo Mkuu,
 Roho yangu na ikuimbie
 Jinsi Wewe ulivyo Mkuu.

[V3]
 Nikitembea pote duniani,
 Ndege huimba, nawasikia,
 Milima hupendeza macho sana,
 Upepo nao nafurahia.

[V4]
 Nikikumbuka kama Wewe Mungu
 Ulivyompeleka Mwanao,
 Afe azichukue dhambi zetu,
 Kuyatambua ni vigumu mno.

[V5]
 Yesu Mwokozi utakaporudi
 Kunichukua kwenda Mbinguni,
 Nitashukuru na kuimba milele,
 Wote wajue jinsi ulivyo.</lyrics>
<title>Bwana Mungu, Nashangaa Kabisa TZR114</title>
<hymn_number>114</hymn_number>
</song>